5 Novemba 2025 - 14:40
Source: ABNA
Mamdani achaguliwa Meya wa kwanza Mwislamu wa Jiji la New York katika ushindi wa kihistoria

Zohran Mamdani mbunge Muislamu amechaguliwa kuwa Meya wa 111 wa jiji la New York, mtu wa kwanza mwenye asili ya Asia Kusini na wa kwanza aliyezaliwa barani Afrika kuongoza jiji kubwa zaidi nchini Marekani.

Mamdani mwenye umri wa miaka 34 na mbunge kutoka Queens aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha jana kwa ajili ya kulioongoza jiji la New York baada ya kuhitimishwa upigaji kura katika mchuano mkali uliovutia hisia na fikra wa waliowengi.

Mamdani amemshinda mpinzani wake mkuu gavana wa zamani Andrew Cuomo kwa kuibuka ushindi wa kura zisizopungua asilimia 50 kati ya jumla ya asilimia 85 ya kura zilizohesabiwa. 

"Tuko kwenye ukingo wa kuweka historia katika jiji letu. Katika ukingo wa kuaga siasa za zamani. Siasa ambazo zinakuamuru mambo yasiyotekelezeka." Ni matamshi ya Mamdani muda mfupi kabla ya kuibuka na ushindi. 

Mbunge huo Mdemocrat ameahidi kusimamia masuala ya kodi na usafiri wa mabasi bila malipo katika jiji la New York.

Takwimu zinaonyesha kuwa, msimamo wa Zohran Mamdani kuhusu Israel na Palestina umemsaidia pakubwa kuvuka katika mchuano wa awali wa kura licha ya kushutumiwa kutoa maoni ya kuwakosoa Wazayuni kuhusu vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza.

Your Comment

You are replying to: .
captcha